WAKUU WA SHULE TRANS NZOIA WASHUTUMIWA KWA KUPANDISHA VIWANGO VYA KARO.

Viongozi kutoka Kaunti ya Trans-Nzoia wamelalamikia hatua ya walimu wakuu kwenye shule mbalimbali Kaunti hiyo kuitisha karo ya juu na mallipo mengine ya ziada kwa wazazi wanapowapeleka wanao kujiunga na shule za upili kinyume na maagizo ya waziri wa elimu Prof George Magogha.
Wakiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge la Kaunti ya Trans-Nzoia ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Endebes Patrick Kisiero wamesema wazazi wengi Kaunti hiyo wanapitia hali ngumu ya maisha kuhakikisha wanao wanajiunga na shule za upili kutokana na malipo hayo ya juu.
Aidha Kisiero amemtaka mkurugenzi wa elimu Betty Maina na Kamishina wa Kaunti ya Trans-Nzoia Sam Ojwang’a kuitisha mkutano wa dharura na wakuu hao ili kutatua swala hilo akisema hatua hiyo huenda ikahujumu sera ya serikali ya kuhakikisha asilimia moja ya wanafunzi wanajiunga na kidato cha kwanza.