WAKUU WA SHULE ENEO LA KIPKOMO WAANZISHA MIKAKATI YA KUZUIA MIGOMO SHULENI.


Walimu wakuu katika eneo la kipkomo eneo bunge la Pokot kusini kaunti hii ya Pokot magharibi wameanzisha mikakati ya kuhakikisha kuwa wanakabili visa vya migomo shuleni ambavyo vimepekelea uharibifu wa mali za shule nyingi.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya St Peters Kapchemogen ambayo ni moja ya shule ambazo mabweni yake yaliteketea mwaka huu Evans mahindu, wapo wanafunzi wengi ambao wanalizimika kulipia gharama ya uharibifu wa mali katika shule hali hawakuhusika katika migomo hiyo, hatua ambayo imewalazimu kuanzisha mikakati ya kuwaelimisha wanafunzi dhidi ya migomo hiyo.
Wakati uo huo mahindu amewataka wazazi na wadau katika shule hiyo hasa wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kuripoti katika shule hiyo mwezi july kutohofu kwani mipangilio mwafaka imewekwa kuhakikisha shughuli ya kuwapokea wanafunzi hao haiathiriwi.
Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya mseto ya chepareria John Cheruo amesema tayari wamezuru shule mbali mbali eneo hilo na kutoa ushauri kwao dhidi ya migomo na badala yake kutafuta mbinu ya kutatua matatizo yanayowakabili ikiwemo kuandaa mazungumzo na wadau husika.