WAKULIMA WATAKIWA KUWA WAANGALIFU DHIDI YA MBEGU GHUSHI

Wakulima kaunti hii ya Pokot Magharibi na taifa jirani la Uganda wametakiwa kuwa waangalifu msimu huu wa upanzi dhidi ya kununua mbegu ghushi ambazo zinauzwa na wafanyibiasha walaghai.

Akizungumza na kituo hiki meneja wa kampuni ya mbegu ya simlaw  tawi la Uganda Ronny Isumba amesema zipo mbegu nyingi ghushi sokoni zenye jina la kampuni hiyo  hivyo wakulima wanapasa kununua mbegu hizo kutoka kwa wafanyibiashara wanaotambulika ili kuepuka kutapeliwa.

Aidha ametoa wito kwa wakulima kutoka maeneo ambako mbegu hizo hazijafika kuwasiliana na kampuni hiyo ambayo ni mshirika wa kampuni mbegu kenya seed  ili kuhakikisha kuwa wanapata mbegu hizo msimu wa upanzi unapoanza.