WAKULIMA WATAKIWA KUKUMBATIA MBUZI WA KISASA AINA YA GALA GOATS.

Wakulima katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kukumbatia mbuzi wa kisasa aina gala goats ili kuimarisha mazao yao.
Akizungumza eneo la Nasukuta wakati wa kupeanwa mbuzi hao kwa makundi 27 ya wakulima, waziri wa kilimo na mifugo kaunti hii Geofrey Lipale amesema kuwa mbuzi hao wana mazao tele na ikilinganishwa na wale wa kienyeji pamoja hali kuwa wanachukua muda mfupi kukua.
Mshirikishi wa mradi wa kilimo wa Kenya climate smart ambao unaendeleza shughuli ya kutoa mbuzi hao kwa wakulima Philip Ting’aa amesema kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuhakikisha kuwa mkulima anawezeshwa kupitia kuimarishwa mazao yake.

[wp_radio_player]