WAKULIMA WATAKIWA KUKUMBATIA KONDOO AINA YA DOPPER.
Wakulimakatika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kukumbatia ufugaji wa kondoo aina ya Dopper.
Akizungumza eneo la siyoi kaunti hii ya Pokot magharibi katika shughuli ya kutoa kondoo hao kwa makundi ya wakulima mshirikishi wa mradi wa kilimo wa kenya climate smart kaunti hii Philip Ting’aa amesema ufugaji wa kondoo hao utawaimarisha pakubwa kibiashara ikilinganishwa na kondoo wa kawaida.
Ting’aa amesema makundi mawili yamenufaika katika mradi huo ambao uko kwenye awamu yake ya pili likiwemo lile la Paraywa silk group na lile la chomyet self help group ambayo yamepokea jumla ya kondoo 61 huku makundi 11 yakilengwa katika wadi hiyo ya Siyoi, wakilenga pia wafugaji wa kuku na ng’ombe.
Wakulima katika makundi ambayo yamenufaika na kondoo hao wakiongozwa na Mike Kiptoo wamepongeza mradi huo ambao wamesema kuwa utawafaa zaidi hasa katika kuimarisha hali yao ya kiuchumi.