WAKULIMA WATAKA BEI ZA PEMBEJEO KUSHUSHWA KAUNTI YA TRANSNZOIA
Wakulima katika kaunti ya transzoia wameadhirika sana na hali mbaya ya hewa ambayo imedhiri upanzi na uzalishaji wa chakula katika kaunti hiyo.
Wakulima kutoka kijiji cha kapsitwet ambao wanajihusisha na ukuzaji wa mahindi wamesema kwamba kwa muda wa miaka miwili sasa hawajavuna mahindi kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma
Wakulima hao aidha wanalaumu kupanda kwa bei ya mbolea kuwa ni mojawapo ya hali amabyo imechagia kushuka kwa mavuno yao ya mahindi
Wataaluamu wa kilimo katika kaunti hiyo wanadadisi kuwa huenda nchi nzima ikakumbwa na uhaba wa chakula ikizingatiwa kuwa kiwango cha mazao ya imeshuka kwa asilimia 15 wataalamu hao wanaongeza kuwa kupanda kwa bei ya pembejeo za ukulima kama mbolea kunamaanisha kuwa wakulima hawatatumia kiwango kinachohitajika cha pembejeo hizo