WAKULIMA WATAHADHARISHWA DHIDI YA KUNUNUA MBEGU GHUSHI.

Wakulima nchini wameshauriwa kununua mbegu zao katika maduka na maajenti walioidhinishwa na kampuni ya mbegu nchini Kenya seed kama njia moja ya kukabili matapeli wanaosambaza mbegu ghushi kwa wakulima nchini.
Akizungumza katika kikao na wanahabari mjini Kitale, afisa wa mauzo katika kampuni ya Kenya seed William Kiberen amesema wanaendeleza elimu kwa wakulima kuhusu baadhi ya nembo za kiusalama kwenye mbegu, mbali na kuwahamasisha kuweka vyema mifuko na risiti ili kutumiwa iwapo kutashuhudiwa na matatizo yoyote kuhusu mbegu za kampuni hiyo.
Wakati huo huo Kiberen amesema kampuni hiyo kwa ushirikiano na asasi zingine za serikali kama kephis na idara ya kukabiliana na bidhaa ghushi wameweka nembo za kiusalama kwenye mifuko ya mbegu mbali na kufanya uchunguzi na kuwanasa matapeli wanaouzia wakulima mbegu ghushi.

[wp_radio_player]