WAKULIMA WALALAMIKIA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA


Hisia kali zimeendelea kutolewa nchini kufuatia tangazo la mamlaka ya kudhibiti bei ya mafuta na kawi nchini EPRA la kuongeza bei ya mafuta.
Kulingana na wakulima katika kaunti ya Trans Nzoia ni kinaya kwa serikali kutofungua bodi ya kitaifa ya mazao na nafaka nchini kununua mahindi waliyohifadhi katika maghala yao na kukosa kuwasambazia mbolea na mbegu kutoka kwa Ncpb hali inayoongeza bei ya diseli ambayo inatumika na trekta kulima hivyo kupandisha gharama ya ukulima.
Aidha wamesema huenda hatua hiyo ikawaathiri wanafunzi ambao wanategemea mafuta taa kwa ajili ya kujiandaa kwa mitihani ya KCPE na KCSE.