WAKULIMA WAITAKA SERIKALI YA POKOT KUWASAMBAZIA PEMBEJEO KWA WAKATI


Huku wakulima wakiendelea kujitayarisha kwa msimu wa upanzi wakazi wa wadi ya Kodich kaunti hii ya Pokot Magharibi wametoa wito kwa serikali ya kaunti kuharakisha mikakati ya kuwasambazia wakulima pembejeo hitajika kwa wakati ufaao.
Wakizungumza na wanahabari, wakulima hao wameitaka wizara ya maji katika serikali ya kaunti kuangazia malalmishi yao kuhusiana uhaba wa maji hali inayotokana na hali ya kiangazi na pia kutorekebishwa kwa shimo za maji zilizoharibika tangu ziliyochimbwa .