WAKULIMA WAHIMIZWA KUKUMBATIA KILIMO CHA KAHAWA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Wakulima katika kaunti ya Pokot magharibi wamehimizwa kupanda kahawa kwa wingi ili kujiimarisha kimapato kando na kuhakikisha uchumi wa kaunti hii unaimarika.
Akizungumza eneo la Tartar wakati wa mafunzo kwa wakulima kuhusu jinsi ya kutekeleza kilimo Cha kahawa katika mpango ulioendelezwa kwa ushirikiano na shirika la world vision, naibu gavana Robert komole amesema kilimo Cha kahawa kina manufaa makubwa.
Aidha Komole amesema serikali ya kaunti itahakikisha ushirikiano Bora na vyama vya ushirika ili kuwanufaisha pakubwa wakulima wa kahawa.
Kwa upande wake afisa katika shirika la world vision Elijah Korir ametoa wito kwa wakulima waliohudhuria mafunzo hayo kuyatilia maanani na kuhakikisha kwamba wanayatekeleza ili kuimarisha kilimo Cha kahawa akiahidi ushirikiano mkamilifu kutoka kwa shirika Hilo.