WAKULIMA WAHIMIZWA KUJIANDAA KWA MSIMU WA UPANZI POKOT MAGHARIBI.

NA BENSON ASWANI
Wakulima katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kujiandaa kwa ajili ya kilimo msimu wa upanzi unapotarajiwa kuwadia.
Ni wito wake wa afisa mkuu katika wizara ya kilimo, mifugo, uvuvi na unyunyiziaji maji mashamba Samason Nyangaluk ambaye aidha amesema wizara yake iko tayari kushirikiana na wakulima kuhakikisha kuwa kilimo chao kinafanikiwa.
Aidha Nyangaluk amesema kuwa shughuli ya kuchanja mbuzi inaendelea katika wadi tatu za eneo la pokot kaskazini akiwataka wagugaji kuhakikisha wanawapeleka mbuzi wao kupewa chanjo ili kuzuia magonjwa ambayo huenda yakawapelekea hasara.