WAKULIMA WAHADAIWA NCHINI NA SERKALI KUU
Mgombea kiti cha ubunge kwa chama cha UDA Wesley Kipchumba Korir ameisuta serikali kuu kupitia kwa wizara ya Kilimo kwa kuwahadaa wakulima wa mahindi nchini.
Akihutubia wenyeji eneo bunge hilo Korir ameshutumu serikali kwa kutoa shilingi Bilioni 5 kuagiza mahindi kutoka mataifa ya kigeni huku wakulima wa mahindi wakikosa soko la zao hilo humu nchini.
Aidha Korir amekosoa mbunge wa sasa kwa kutenga fedha kidogo kwa ufadhili wa watoto kutoka jamii maskini eneo hilo akiwamewarai wenyeji wa eneo hilo kumpa nafasi katika uchaguzi ujao ilikushughulikia vyema maswala ya masomo kwa wanao baada ya uchaguzi was Agosti 9.