WAKULIMA WAFURAHIA MBOLEA YA BEI NAFUU TRANS NZOIA.


Wakulima Kutoka Kaunti ya Trans Nzoia wameelezea furaha yao kuhusu serikali kuu kutoa kwa mbolea ya bei nafuu ya shilingi 3500 kwa kila gunia ya kilo 50 ya mbolea.
Wakihutubu  mjini Kitale wakiongozwa na Fredrick Rono wakulima hao wamaesema hii itakuwa nafuu kwa wakulima ambao wanakuza mimea ya muda mfupi msimu huu, wakitaka serikali kuweka mikakati ya kutafuta suluhu ya kudumu kwa swala la mbolea nchini.
“Mbolea hii ni afueni kwetu ikizingatiwa tumekuwa tukinunua mbolea kwa bei ya juu mno. Sasa tutapata wakati mzuri wa kupanda mimea inayochukua muda mfupi kukomaa.” Alisema
Aliongeza kwa kusema, “hii ni mbolea ya muda mfupi ingekuwa vizuri kama serikali ya rais William Ruto ingeweka mikakati ya kupata suluhu ya kudumu kuhakikisha kwamba bei ya mbolea inasalia chini. Hata hivyo tunashukuru kwa hatua hii nzuri.”
Wakati huo huo Rono ameitaka serikali mpya  ya Kenya Kwanza kuhakikisha mbolea inapatika kwa wingi katika maghala ya NCPB mbali na kupunguzwa kwa masharti yanayotolewa kwa wakulima kabla ya kupata mbolea hiyo.
“Kuna masharti mengi ambayo yanaambatana na mbolea hii. Japo tumefurahia lakini ni vyema kama masharti hayo yangepunguzwa, na serikali ihakikishe mbolea hiyo inapatikana kwa wingi.” Alisema.

[wp_radio_player]