WAKULIMA WA NYASI WANUFAIKA NA UFADHILI KUTOKA SHIRIKA LA NRT.


Shirika la NRT limetoa kilo 600 za mbegu ya nyasi kwa wakulima ambazo zinanuiwa kupandwa katika ekari 60 eneo la Masol kaunti ya Pokot magharibi.
Akizungumza baada ya kukutana na wakulima hao eneo la Masol, mkurugenzi wa shirika hilo Rebecca Kochulem amesema kuwa hatua hii itawasaidia wakulima hao kuongeza mapato yao kupitia kupanda nyasi.
Aidha Kochulem amesema kuwa wanalenga kutoa mafunzo kwa wakulima hao kuhusu jinsi ya kukuza nyasi ili kuongeza uzalishaji pamoja na kuwatengenezea sehemu ya kuhifadhi nyasi hizo.
Wakati uo huo amesema kuwa shirika la NRT linashirikiana na wadau wengine kama shirika la E- for impact ambalo litahusika na kuwafunza pamoja na kutafuta soko kwa ajili ya mazao ya wakulima hao.