WAKULIMA WA NYANYA KAUNTI YA TRANS NZOIA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA VYAMA VYA USHIRIKA
Wito umetolewa kwa wakulima wa nyanya kaunti ya Trans-nzoia kujiunga katika ushirika ili kuzungumza kwa sauti moja na kupigania bei bora kwa wakulima wanaokuza zazo hilo katika kaunti hiyo.
Akihutubu eneo la Kiptogot mwakilishi wadi ya chepchoina eneo bunge la Endebess Evans Chesang amesema hatua hiyo itatoa suluhu ya kudumu na kuwazuia madalali ambao wamekuwa wakiwapunja wakulima wa zao hilo kwa muda mrefu kwa kukosa ufahamu wa soko la bidhaa zao.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na mwenyekiti wa chema tomato co-operative Joseph Maingi Ngunjiri akisema kupitia kwa muungano huo wamepata kutia sahini mkataba wa maelewano na shirika moja kwa jina M-shamba ambalo linanunua nyanya kutoka kwa wakulima kwa shilingi 50 kwa kilo moja, jambo ambalo ametaja kuwa limeleta afueni kwa wakulima eneo hilo.