WAKULIMA WA KAHAWA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUKUMBATIA KILIMO BIASHARA.


Wakulima wa kahawa Kaunti hii ya pokot magharibi waliweza kuzalisha takriban kilo 170,000 kutoka kwa wakulima mwaka uliopita, ambazo tayari zimewasilishwa kwenye mnada wa kahawa na wamepokea malipo.
Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa vyama vya ushirika kaunti hii ya pokot magharibi Samson kamarich ambaye aidha amewataka wakulima kuweka mbolea kwenye mashamba yao haswa msimu huu wa kiangazi ili kuboresha uzalishaji wa mazao.
Amewarai wakulima kuboresha ukulima wao na kukumbatia kilimo biashara ili kuinua mapato yao na kuimarisha ukuzaji wa kahawa ikiwa ni njia moja wepo ya kuinua uchumi kwa wakulima, wakati uo huo akiitikia mpango wa gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo wa kuwapa wakulima miche ya kahawa.