WAKULIMA WA ASALI KUNUFAIKJA ZAIDI NA MIKAKATI YA SERIKALI POKOT MAGHARIBI.
Serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wakulima wa asali wanalindwa dhidi ya madalali ambao wamekuwa wakipunja kwa muda wakulima wa zao hilo.
Akizungumza wakati wa kikao na wadau yakiwemo mashirika mbali mbali yasiyo ya serikali likiwemo la GIZ waziri wa biashara viwanda kawi na vyama vya ushirika kaunti hii ya pokot magharibi Francis Kitalawian amesema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakikadiria hasa kutokana na kutapeliwa mazao yao na madalali hao.
Kitalawian amesema kuwa ili kuzuia hali hii serikali ya kaunti kupitia idara ya biashara na viwanda inawekeza zaidi katika mashirika mbali mbali ya kibiashara ambako wakulima hao watakuwa wakiuza asali yao ambapo watakuwa wakilipwa fedha zao papo kwa hapo.