WAKULIMA TURKWEL WANUFAIKA NA MIZINGA.


Shirika la safer kwa ushirikiano na mashirika mengine matano ikiwemo lile la NRT limetoa mizinga pamoja na vifaa vingine vitakavyotumika kuvuna asali kwa wakulima wa asali eneo la Turkwel katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Akizungumza baada ya kutoa vifaa hivyo afisa katika shirika hilo Tadius Ombati amesema kuwa mbali na kutoa vifaa hivyo kwa wakulima, wametoa mafunzo ya jinsi ya kukuza asali kwa wakulima hao lengo kuu likiwa kuhakikisha kuwa wanawezeshwa zaidi pamoja na kuvuna asali bora na yenye viwango vya juu.
Mkurugenzi wa idara ya uzalishaji wa mifugo katika kaunti hii ya pokot magharibi Paul Richong’er amepongeza mradi huo ambao amesema kuwa unaambatana na malengo ya serikali ya kaunti hii kuhakikisha kuwa mkulima ana chakula cha kutosha pamoja na kuwezeshwa kiuchumi.
Kwa upande wake chifu wa Kositei Asiroi Afrikano amewahimiza wakulima kutumia vyema vifaa hivyo ambavyo wamepewa na mashirika hayo kwa kuzingatia elimu ambayo wamepewa ili kunufaika na kujikimu kimaisha kupitia kilimo cha ufugaji wa nyuki.
Wakulima hao wamepongeza juhudi za shirika hilo kuhakikisha wanwezeshwa kiuchumi wakiahidi kutumia mfuzo waliyopewa ili kuimarisha kilimo hicho.