WAKULIMA TURKWEL NA LOIMA WAKUMBATIA MBINU MPYA ZA KILIMO.


Wakulima kutoka eneo la Turkwel na Loima Turkana kusini wamekumbatia mbinu mpya ya upanzi wa mimea kwenye mifuko uliowekwa mchanga wenye rutuba ili kuepuka hasara ambayo wamekuwa wakikadiria kutokana na ukame.
Baadhi ya wakulima hao wamesema kuwa wamekuwa wakipata mapato duni katika kilimo chao kutokana na uhaba wa maji ambao unashuhudiwa eneo hilo kila mara.
Kulingana na wataalam kutoka shirika la pan Africa ambalo linawasaidia wakulima kutekeleza mradi huo, tayari mbinu hiyo ya kilimo imeanza kuwa na manufaa kwa wenyeji wa maeneo yanayokumbwa na uhaba wa maji.
Aidha wakulima wamewataka viongozi wa siasa kutoka maeneo hayo kuwahimiza vijana kujiingiza katika kilimo hicho wakati wanapoendeleza kampeni zao ili kukabili njaa ambayo inashuhudiwa kaunti ya Turkana kila mara.