WAKULIMA TRANS NZOIA WATAKIWA KUWA MACHO KUHUSIANA NA UVAMIZI WA VIWAVI JESHI.


ya kilimo katika kaunti ya Trans nzoia imeonya kuhusu uwepo wa viwavi jeshi katika baadhi ya maeneo na kuwataka wakulima kuhakikisha wanaripoti visa hivyo mapema endapo vitatokea.
Waziri wa kiliimo kaunti hiyo mary nzomo anasema tayari serikali ya kaunti imenunua dawa ya kuwanyunyizia wadudu hao ili kuwasitiri wakulima kutokana na hasara.
Nzomo anasema uwepo wa wadudu hao huenda ikasambaratisha juhudi za wakulima kuzalisha chakula cha kutosha, jambo ambalo ametaja kuwa hatari kwa usalama wa chakula nchini.
Aidha baadhi ya wakulima katika eneo la kiminini wameelezea masikitiko yao kutokana na hasara ambayo wamekumbana nayo kufuatia kuzuka kwa viwavi jeshi katika baadhi ya maeneo.