WAKULIMA TRANS NZOIA WATAKIWA KUKUMBATIA MPANGO WA WAREHOUSE RECEIPT SYSTEM.

Na Benson Aswani
Wito umetolewa kwa wakulima Kaunti ya Trans Nzoia Kukumbatia Mpango wa serikali wa kuhifadhi nafaka katika maghala bodi ya nafaka na mazao nchini NCPB chini ya mpango wa warehouse receipt System ili kuzuia uharibifu wa mazao yao kutokana na mvua kumbwa inayoendela kushuhudiwa kaunti hiyo.
Akihutubu mjini Kitale mmoja wa viongozi Kaunti hiyo Boniface Wanyonyi amesema wakulima nchini hupoteza asilimia thelathini ya mazao yao kutokana na mabadiliko ya hali ya anga wakati wa mavuno, akisema mpango huo wa serikali utawasaidia wakulima kupata huduma ya kukausha mazao yao mbali na kuhakikisha usalama wa nafaka zao.
Wanyonyi ambaye ametangaza nia ya kugombea kiti cha ugavana ameelezea kughadhabishwa na hali ya umasikini Kaunti hiyo ya Trans Nzoia licha ya kuwa ndiyo ghala kuu la chakula nchini, akisema kuwa akipewa nafasi ya uongozi wa kaunti hiyo ataweka mikakati ya kukabiliana na ongezeko na umasikini miongoni mwa wakazi mbali na kuimarisha uchumi.