WAKULIMA TRANS NZOIA WAPUUZILIA MBALI BEI MPYA YA MAHINDI.


Baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Trans nzoia wamepuuzili mbali bei mpya ya mahindi ambayo ilitangazwa na waziri wa kilimo Peter Munya wakisema kuwa ni ya chini mno ikilinganishwa na gharama ya uzalishaji.
Wakiongozwa na mwanasiasa Alwin Sasia, wanasiasa hao wameitaka serikali kutangaza bei mpya ambayo itamfaidi mkulima, kwani ilivyo sasa mkulima atakadiria hasara kubwa iwapo bei itasalia jinsi alivyotangaza waziri Munya.
Wakati uo huo Sasia amemtaka waziri Munya kutangaza kushuka bei ya mbolea na kuwahakikishia wakulima upatikanaji wa mbolea hiyo kwani mara nyingi ni mabwenyenye ambao hunufaika na mbolea hiyo.

[wp_radio_player]