WAKULIMA TRANS NZOIA WAPONGEZA UTEUZI WA MKURUGENZI MPYA WA KAMPUNI YA KENYA SEED.

Na Benson Aswani
Wakulima kutoka Kaunti ya Trans Nzoia wamepongeza uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya mbegu nchini Kenya Seed Fred Oloibei uteuzi uliofanyika juma lililopita na waziri wa kilimo Peter Munya kupitia kwa gazeti rasmi la serikali na kuchukua hatamu kutoka kwa aliyekuwa mkurugenzi Azaria Soy.
Wakiongozwa na Fredrick Rono wakulima hao wamemtaja Oloibei kama kiongozi mchapa kazi na aliye na tajriba ya muda mrefu kuhusu ukuzaji wa mbegu katika shirika hilo.
Aidha Rono ametoa wito kwa mkurugenzi huyo mpya kuimarisha zaidi shirika hilo la kitaifa la mbegu kwa kuwekeza zaidi katika utafiti wa mbegu ili kupiga jeki kilimo cha zao la mahindi ambayo ni moja wapo ya ajenda kuu za rais Kenyatta ya utoshelezaji wa chakula nchini.