WAKULIMA TRANS NZOIA WAELEZEA HOFU YA KUSAJILI HASARA MSIMU HUU.


Baadhi ya wakulima wa mahindi katika kaunti ya trans nzoia wameelezea wasi wasi wa kusajili hasara kubwa pindi watakapovuna mazao yao mwishoni mwa mwaka huu.
Wakulima hao wamesema kuwa wengi wao walilazimika kutumia kiwango kidogo cha mbolea wakati wa upanzi kutokana na gharama ya juu ya bidhaa hiyo muhimu.
Fredrick rono ambaye ni mmoja wa wakulima hao amesema kuwa uzalishaji wa mahindi kaunti hiyo mwaka huu huwenda ukapungua kwa asimilia 40 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Rono aidha anailaumu wizara ya kilimo chini ya waziri peter munya kwa kufeli kuwasambazia wakulima mbolea yenye ruzuku kwa wakati ufaao kama miaka ya hapo awali.