WAKULIMA SIYOI WAFUNZWA UMUHIMU WA KILIMO HAI.


Wakulima katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kunufaika na mafunzo kutoka mashirika mbali mbali kuhusu mbinu za kilimo katika juhudi za kuhakikisha wanazingatia kilimo bora na kukabili baa la njaa.
Akizungumza eneo la siyoi baada ya kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu kilimo hai yani organic farming kilimo kinachohusu matumizi ya mbolea ya asili, afisa kutoka shirika la kilimo la biodiversity and biosafety association of Kenya Ann Maina amesema kuwa aina hii ya kilimo inahakikisha usalama wa chakula kwani mkulima hatolazimika kutumia dawa ambazo ni hatari kwa afya.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na kennedy kiptoo ambaye amekuwa akiendeleza kilimo hicho.
Afisa kutoka wizara ya kilimo kaunti hii ya Pokot magharibi Benard Misiko amewataka wakulima kukumbatia mbinu hiyo ya kilimo kwani itahakikisha usalama wa chakula pamoja na utoshelevu wa chakula ambayo ni moja ta ajenda kuu za serikali.
Ni mafunzo ambayo yamechangamkiwa na baadhi ya viongozi kaunti hii wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Lomut Jcob Ang’olemuk pamoja na wakulima wakisema ni kilimo cha gharama ya chini na kitakachopelekea viwango vya juu vya mavuno iwapo kitakumbatiwa na wakulima.