WAKULIMA POKOT MAGHARIBI WATAHADHARISHWA KUFUATIA UCHACHE WA MVUA.


Wakulima katika kaunti hii ya Pokot Magharibi wameshauriwa kuchukua tahadhari kutokana na ukosefu wa mvua kwa takriban miezi mitatau sasa.
Waziri wa kilimo na mifugo katika kaunti hii ya Pokot Magharibi Lipale Geoffrey, amesema kuwa kwa sasa hali ya anga si nzuri huku akionya kwamba huenda tukakosa mvua kwa mda.
Akizungumza na kituo hiki Lipalee aidha mewataka wakulima kuchunga chakula ambacho wako nacho kwa sasa huku akisema kuwa huenda tusipokee mvua ya kutosha hivi karibuni.
Kadhalika Lipalee amewataka wakulima kutoachilia mifugo wao kula mimea ambayo iko kwenye mashamba yao ambayo huenda imearibika huku akitoa wito kwa serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba inatenga fedha ya kutosha ya kuwalinda wananchi.