WAKULIMA POKOT MAGHARIBI WASHAURIWA KUTAYARISHA MASHAMBA YAO HUKU MVUA IKITARAJIWA KUANZA HIVI KARIBUNI


Wakulima katika kaunti hii ya Pokot magharibi hasa kutoka nyanda za juu wametakiwa kuendelea kuandaa mashamba yao kwa msimu wa upanzi mvua inapotarajiwa kuanza kushuhudiwa maeneo hayo.
Haya ni kulingana na mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti hii Wilson Lonyangole ambaye amesema huenda maeneo kadhaa ya kaunti hii yakaanza kupokea mvua kuanzia juma la pili la mwezi huu hadi juma la tatu.
Aidha Lonyangole ameishauri idara ya majanga kuandaa wakazi ambao wanaishi maeneo ambako kuna uwezekano wa kushuhudiwa maporomoko ya ardhi ili kuzuia maafa ambayo huenda yakatokea msimu wa mvua utakapoanza.
Wakati ou huo Lonyangole ametoa wito kwa maafisa katika idara ya afya kuweka mikakati ya kuzuia mkurupuko wa magonjwa kama vile kipindupindu na malaria katika kipindi hiki.