WAKULIMA POKOT MAGHARIBI WAENDELEA KUIMARIKA CHINI YA MRADI WA KENYA CLIMATE SMART.

Mradi wa Kenya climate smart umeendeleza harakati za kuyawezesha makundi mbali mbali ya wakulima kaunti ya Pokot magharibi kuimarisha kilimo chao hasa kinachohusu ufugaji na kilimo cha mimea.

Msirikishi wa mradi huo kaunti ya Pokot magharibi Philip Ting’aa alisema hadi kufikia sasa zaidi ya makundi 400 ya wakulima wamenufaika chini ya mradi huo ikiwemo wanaotekeleza kilimo cha mtama na ndengu.

Aidha Ting’aa alisema kwamba makundi hayo yamenufaika na ng’ombe wa maziwa, mbuzi aina ya gala ambao wanastahimili makali ya ukame pamoja na kondoo aina ya Dopper. 

“Kufikia sasa tumeweza kusaidia makundi 483 ya wakulima ambao wamenufaika kwa ng’ombe wa maziwa, mbuzi aina ya gala ambao wanastahimili kiangazi na pia kondoo aina ya doper. Aidha wakulima wanaokuza mtama na ndengu wamenufaika kupitai mradi huu.” Alisema Ting’aa.

Alisema kwamba shilingi milioni 356 zimetumika katika mradi huu kufikia sasa.

Jumla ya pesa ambazo tumetumia kwa makundi haya ni shilingi milioni 356.” Alisema.

Wakati uo huo Ting’aa alisema wanaendeleza mradi wa kununyizia maji mashamba hasa sehemu kame katika kaunti hiyo ambayo inalenga kuwanufaisha zaidi ya wakulima 500.

“Tumeanza pia kuwa na mradi wa kunyunyizia maji mashamba hasa sehemu za Siyoi unaoitwa Chepkotii irrigation project, na ule wa Kikin eneo la Sook. Miradi hii inalenga kuwanufaisha wakulima zaidi ya 500 hasa kutoka maeneo kame.” Alisema.