WAKULIMA KAUNTI YA UASIN GISHU WATAHADHARISHWA DHIDI YA KUNUNUA PEMBEJEO GHUSHI
Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago amesema kuwa serikali yake itafutilia mbali leseni za wafanyibiashara ambao watapatikana wakiuza bidhaa ghushi kwa wakulima kwenye kaunti hiyo na hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao..
Akizungumza na wanahabari Mandago amesema kuwa lengo kuu la hatua hiyo ni kuangamiza biashara hiyo kwenye eneo hilo.
Mandago aidaha maesema kuwa iwapo wakulima watanunua pembejeo ghushi za kupanda uzalishaji wa chakula utaathirika humu nchini.
Mwenyekiti wa mamlaka ya kupambana na bidhaa ghushi nchini Flora Mutahi kwa upande wake amewataka wakulima kununua bidhaa zao kutoka kwa maduka yaliyoidhinishwa ili waweze kupata bidhaa halali.