WAKULIMA KAUNTI YA TRANS NZOIA WALALAMIKIA KUPANDA GHARAMA YA KILIMO


Viongozi kaunti ya Trans-nzoia wanamtaka waziri wa kilimo Peter Munya na kamati ya kushughulikia maswala ya kilimo katika bunge la kitaifa kuingilia kati na kuwanusuru wakulima kutokana na kupanda maradufu kwa gharama ya kilimo nchini.
Wakiongozwa na John Njuguna kutoka eneo bunge la Cherangani wamesema bei ya mbolea na mbegu imepanda maradufu akiongeza kuwa wakulima wengi wanapitia hali ngumu ya kiuchumi kutoka na janga la covid 19.
Aidha Njuguna ameitaka kamati ya bunge la kitaifa kuhusu kilimo ikiongzwa na mbunge wa moiben silas tiren kuingilia kati na kuhakikisha serikali inapunguza bei ya bidhaa hizo pamoja na mafuta na kuhakikisha wakulima wanapata mbolea katika maghala ya (ncpb).
Njuguna ambaye ametangaza kuwania kiti cha eneo bunge la cherangani anahofia kutokuafikiwa kwa ajenda ya utoshelezi wa chakula nchini iwapo serikali haitaingilia kati na kupunguza gharama ya ukulima nchini.