WAKULIMA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUWA NA SUBIRA MAOMBI YAO YAKISHUGHULIKIWA.


Makundi ya wakulima katika kaunti hii ya pokot magharibi yaliyotuma maombi ya kunufaika na mradi wa climate smart yametakiwa kuwa na subra wakati maafisa katika mradi huo wakishughulikia maombi yao.
Akizungumza baada ya kikao na maafisa katika mradi huo, mshirikishi wa mradi huo wa climate smart kaunti hii Philip Ting’aa amesema kuwa wametenga shilingi milioni 96 zitakazotumika katika kuwanufaisha wakulima kutoka makundi 116 wakilenga kufikia zaidi ya makundi 500.
Aidha Ting’aa ametoa wito kwa wakulima ambao watanufaika katika mradi huo kuhakikisha kuwa wanatunza vyema vifaa watakavyopokea pamoja na kuhakikisha mbegu za mifugo wanazopewa zinawanufaisha wakulima zaidi ili kufanikisha kilimo cha ufugaji kaunti hii.