WAKULIMA ELGEYO MARAKWET WAKADIRIA HASARA KUFUATIA UVAMIZI WA NDOVU.


Wakulima katika wadi ya Endough kaunti ya Elgeyo Marakwet wanakadiria hasara baada ya ndovu kuvamia mashamba yao na kuharibu mimea.
Wakiongozwa na Nickson Chongwony, wakulima hao wamesema ndovu hao wamekuwa wakiwahangaisha kwa takriban mwezi mmoja wakiharibu mimea yao mashambani hali wanayosema imewasbabishia hasa huku wakitaka shirika la wanyamapori KWS kuingilia kati upesi.
Katibu wa utawala katika wizara ya utalii na wanyamapori Joseph Boinet amekiri kuwepo visa vya uvamizi wa ndovu kwenye maeneo ya marakwet masharik, magharibi na keiyo kaskazini katika kaunti ya Elgeyo marakwet hivi karibuni.
Boinet amesema kuwa tayari maafisa wa KWS wamefahamishwa kuhusu uvamizi huo na wanendeleza juhudi za kuwaelekeza ndovu hao kunakostahili.