WAKIMBIZI TRANS NZOIA WALALAMIKIA KUTENGWA KIELIMU.


Siku moja baada ya ulimwengu kuadhimisha siku ya kusoma na kuandika jamii ya wakimbizi wa ndani kwa ndani Kaunti ya Trans Nzoia wamelalamikia ugumu ambao wanao wanapitia kupata elimu .
Kwa mujibu wa mshirikishi wa vuguvugu la Wakimbizi hao kwa jina Integrated IDPs Mark Adir wengi wa watoto kutoka jamii za wakimbizi hao Kaunti ya TransNzoia wamekumbwa na matatizo ya kuendelea na masomo yao kutokana na umasikini na hali ngumu ya kiuchumi mbali na gharama ya juu ya kumudu mahitaji ya wanafunzi shuleni.
Aidha Adir ametoa wito kwa wizara ya elimu kuingilia kati na kuwanusuru watoto wengi kutoka kwa waadhiriwa hao ambao wanafaa kuendelea na masomo yao lakini wanakumbwa na tatizo la ukosefu wa karo, jambo ambalo limechangia wengi kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu.