WAKENYA WASHAURIWA KUZINGATIA MASHARTI YA KUZUIA MAAMBUKIZI ZAIDI YA VIRUSI VYA CORONA


Seneta wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Dkt Samwel Poghisio amewataka wakazi wa kaunti hii kuendelea kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali kwa ushirikiano na wizara ya afya ili kukabili maambukizi ya virusi vya corona humu nchini.
Akizungumza na kituo hiki, Dkt Poghisio hata hivyo amewataka wakazi kuwa waangalifu zaidi hasa wakati huu ambapo kunashuhudiwa wimbi la tatu la virusi hivyo ambalo linakisiwa kuwa huenda likawa baya zaidi.
Dkt Poghisio kadhalika ametumia fursa hiyo na kutoa wito kwa kusuluhishwa kwa mizozo ya mara kwa mara kuhusu ardhi yenye utata ya Chepchoina, akisema kuwa kiako kitaandaliwa hii leo katika eneo hilo ili kutufuta mwafaka kuhusiana na utata huo.