WAKENYA WASHAURIWA KUTOA DAMU KAMA NJIA MOJA YA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE


Kama njia moja ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, wizara ya afya leo hii inatarajiwa kushirikiana na masharika mbali mbali ikiwemo lile la Amref na shirika la msalaba mwekundi ili kukusanya damu.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amewarai wakenya kuhakikisha kwamba wanatoa damu katika vituo vyote ya damu nchini.
Kagwe amesema kuwa wanawake wengi wanaiaga dunia wakati wanajifungua kwa kutokwa damu nyingi akisema kuwa ni miongoni mwa changamoto ambazo zinawakumba na zinastahili kushughulikiwa kwa kuhakikisha kwamba kuna damu ya kutosha katika hifadhi za damu kote nchini.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Choose to Challenge” ambayo inalenga kutafuta mbinu mbali mbali za kutatua changamoyo ambazo zinakumba wanawake.

[wp_radio_player]