WAKENYA WASHAURIWA KUJITOKEZA ILIKUJISAJILI KUWA WAPIGA KURA


Viongozi mbalimbali wanazidi kuwasihi wakenya kujitokeza ndani ya siku thelathini zilizotolewa kusajiliwa kuwa wapiga kura katika kaunti ya Uasingishu.
Wanasiasa hao akiwemo Jackson Mandago ambaye ni gavana wanaendeleza wito huo.
Wakizungumza na wanahabari baada ya kuzinduliwa kwa mpango wa Kusajili Wapiga Kura mshirikishi wa tume ya uchaguzi katika kaunti ya uasingishu jane gitonga amesema maafisa miamoja sitini na sita wametumwa kwenye wadi zote za kaunti kuwasajili wapiga kura.
Aidha maafisa wengine thelathini wametumwa kuwasajili wapiga kura.
Gitonga amewashuri vijana kujitokeza ilikusajiliwa kuwa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao