WAKENYA WASHAURIWA KUENDELEA KUPOKEA CHANJO YA COVID 19


Wito umetolewa kwa wakenya kuhakikishwa wanachanjwa dhidi ya virusi vya corona ambavyo vinaendelea kutikisa taifa hili
Ni wito ambao umetolewa na mbunge wa Soy katika kaunti ya Uasin Gishu Caleb Kositany, ambaye amesema kuwa chanjo dhidi ya virusi hivyo ni bora katika kuzuia maambukizi zaidi
Akiongea katika hafla ya kuchangisha pesa katika kanisa moja la katoliki eneo bunge la Soy, Kositany amewahimiza waliochanjwa kuendelea kufuata masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ili kuzuia msambao wa corona kama vile kunawa mikono na kuvalia barakoa
Hadi kufikia sasa watu 975, 265 wamechanjwa dhidi ya virusi vya corona kote nchini