WAKENYA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPOKEA CHANJO DHIDI YA CORONA.


Viongozi wa kidini chini ya muungano wao wa Trans-Nzoia county inter-religious council of Kenya network wameendelea kuhimiza wakenya kujitokeza kwa wingi ili kupata chanjo dhidi ya covid19.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa muungano huo Raymond Mutama viongozi hao wamesema hatua hiyo itasaidia katika kukabiliana na makali ya ugonjwa huo, akipongeza serikali kwa kulegeza kamba kuhusu utoaji wa chanjo hiyo bila ya kuwalazimisha umma.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na mwenyekiti wa SUPKEM tawi la Trans-Nzoia ambaye pia ni Naibu mwenyekiti wa Trans-Nzoia county inter-religious council of Kenya network Haji Alim ambaye amepongeza serikali kwa juhudi zake kuhakikisha kila mkenya anapata chanjo hiyo, akipuuzilia mbali wanaoeneza uvumi dhidi ya chanjo hiyo.