WAKAZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA MWANAKANDARASI ALIYETWIKWA JUKUMU LA KUJENGA BARABARA KADHAA KAPENGURIA.


Wakazi wa maeneo ya kamwino, chewoyet, sakas hadi eneo la siyoi wametakiwa kushirikiana na mwanakandarasi anayetarajiwa kutekeleza shughuli ya ujenzi wa barabara ya kupitia maeneo hayo unaotarajiwa kuanza karibuni.
Akizungumza kwa niaba ya mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto wakati wa shughuli ya kuwahusisha wananchi katika mipango ya ujenzi wa barabara hiyo, msaidizi wa mbunge huyo Benson kibet amewataka wakazi hao kushirikiana na mwanakandarasi huyo ili kufanya rahisi shughuli hiyo.
Wakati uo huo Kibet amemtaka mhandisi anayesimamia ujenzi wa barabara hiyo kuhakikisha kuwa shughuli hiyo inaafikia viwango hitajika, akimtahadharisha kuwa atawajibishwa iwapo kazi hiyo haitatekelezwa inavyostahili.
Kwa upande wake mhandisi Edwin Limo ambaye ni mkurugenzi wa mamlaka ya KURA eneo la kaskazini mwa bonde la ufa, amewahakikishia wakazi kuwa barabara hiyo ambayo itachukua muda wa miaka miwili kukamilika itajengwa kulingana na viwango vya KURA.