WAKAZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKABILI AJALI ZA BARABARANI TRANS NZOIA.


Wakazi wa kaunti ya Trans nzoia wametakiwa kushirikiana na idara ya trafiki katika kukabili visa vya ajali za barabarani hasa msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya.
Ni wito ambao umetolewa na naibu afisa wa mamlaka ya usalama barabarani NTSA kaunti ya Trans nzoia Cyprian Nyaosi ambaye amewataka wananchi kuwa makini na kuwaripoti madereva ambao wanakiuka sheria za barabarani ili hatua za sheria zichukuliwe.
Nyaosi amesema kuwa ajali nyingi katika kaunti hiyo husababishwa na wahudumu wa boda boda na kufuatia hali hiyo mamlaka hiyo imeanzisha mafunzo kwa wahudumu hao katika juhudi za kuhakikisha kuwa jail zinazosababishwa na sekta hiyo zinakabiliwa.