WAKAZI WATAKIWA KUKUMBATIA MATUMIZI YA CHOO POKOT KUSINI.


Wakazi wa eneo bunge la Pokot kusini kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kukumbatia matumizi ya choo ili kuepuka magonjwa ambayo yanatokana na uchafu.
Ni wito wake afisa wa jamii eneo la pokot kusini kaunti ya Pokot magharibi Julius Kimechwa ambaye aidha amesema kuwa mikakati imewekwa kwa ushirikiano na maafisa walio nyanjani kuhakikisha kuwa kila boma katika eneo bunge hilo wana choo.
Aidha Kimechwa amesema kuwa juhudi za wahudumu wa afya wa kujitolea kwa ushirikiano na machifu pamoja na manaibu wao zimechangia pakubwa kuhakikisha idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo wanachimba na kujenga vyoo.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na afisa wa afya ya umma eneo la Chepareria na Plelakan Lindah Kemboi ambaye pia amepongeza ushirikiano wa wananchi wa eneo hilo ambao umepelekea vyoo kujengwa katika kila boma.