WAKAZI WATAKIWA KUKUMBATIA BARAZA LA MAWAZIRI LA GAVANA KACHAPIN.

Wito umetolewa kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kushirikiana kikamilifu na baraza la mawaziri lililobuniwa na gavana Simon Kachapin ili kuhakikisha utendakazi bora na kujizuia na kuingiza siasa katika mchakato wa uteuzi na uapisho wa mawaziri hao.

Wakiongozwa na Charles Ogaki mkazi wa eneo la Pokot kusini, baadhi ya wakazi walisema kuwa walioteuliwa katika baraza hilo ni wakazi wa kaunti hii na hivyo hamna sababu ya baadhi ya wakazi kukosoa hatua hiyo ya gavana Kachapin.

“Nawaambia wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kwamba nafasi za kazi ambazo zipo katika serikali ya kaunti ni chache mno na wale gavana amewachagua tunafaa kuwakubali. Hamna haja ya kuendeleza siasa na kelele kuhusu wale ambao wameteuliwa. Waliopewa nyadhifa hizo ni watoto wetu.” Alisema Ogaki.

Wakati uo huo Ogaki aliwahimiza wakazi hasa maeneo ya mipakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani za Baringo, Elgeyo Marakwet na Turkana kudumisha amani ili kutoa nafasi kwa utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.

Nataka niwahimize viongozi wetu wa pokot magharibi wakiongozwa na gavana, seneta pamoja na wabunge kwamba tumeumia kwa muda mrefu sana katika kaunti hii na hamna mtu anayejali watu wa chini. Tunaomba kamishina wa kaunti hii kwamba aangazie hali ya usalama ili watu wapate amani.” Alisema.

Aliongeza kwa kusema, “Tunaomba wakazi wa pokot magharibi, Turkana, Baringo na Elgeyo marakwet kwamba tupende amani ndipo tupate maendeleo.”

[wp_radio_player]