WAKAZI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJISAJILI KUWA WAPIGA KURA.


Shughuli ya usajili wa wapiga kura inapoendelea, viongozi katika kaunti hii ya pokot magharibi wameendelea kutoa mwito kwa wakazi kujitokeza kwa wingi kujisajili kuwa wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Akizungumza na kituo hiki mwakilishi kina mama katika kaunti hii Lilian Tomitom amesema ni kupitia njia hiyo tu ambapo wakazi wataweza kutekeleza wajibu wao wa kidemokrasia wa kuwachagua viongozi bora wanaowapendelea.
Wakati uo huo Tomitom ametoa wito kwa viongozi na wataalam mbali mbali kuchukua jukumu la kuwahamasisha wafugaji wa kuhamahama kuhusu umuhimu wa kujisajili kuwa wapiga kura, huku pia akipendekeza kuanzishwa mpango wa kutoa chakula kwa wakazi wanaokabiliwa na njaa ili kuwawezesha kujisajili.
Yanajiri haya huku kaunti hii ya Pokot magharibi ikiorodheshwa miongoni mwa kaunti ambazo zimesajili idadi ya kuridhisha ya wapiga kura katika wiki ya kwanza ya zoezi la usajili wa wapiga kura wapya ambalo linaedezwa na tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC baada ya kusajili wapiga kura 3,585.
Hadi kufikia jana IEBC ilikuwa imesajili jumla ya wapiga kura alfu 202,518, licha ya lkulenga kuwasajili wapiga kura 1,500,000 kwa wiki moja.