WAKAZI WATAKIWA KUJITOKEZA KUJISAJILIWA KUWA WAPIGA KURA ZOEZI HILO LINAPOTAMATIKA.

Na Benson Aswani
Zoezi la kuwasajili wapiga kura wapya linapoendelea kufika tamati, viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kuwahamasisha wakazi hasa vijana kujitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kuwa wapiga kura.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kanisa jipya eneo la mtembur kaunti hii ya Pokot magharibi iliyoongozwa na askofu mkuu wa kanisa katoliki dayosisi ya Kitale Mourice Crowley, mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto amesema ni kupitia usajili huo tu ambapo wakazi watapata fursa ya kuwachagua viongozi wanaowapendelea.
Moroto amesema kuwa muda wa usajili wa wapiga kura hautaongezwa kutokana na mgao finyu ambao ulitengewa tume ya uchaguzi nchini IEBC hivyo vijana hawastahili kusubiri hadi dakika za mwisho kabla ya kujitokeza kusajiliwa.
Kwa upande wake askofu Crowley amesema kuwa juhudi zinaendelezwa na viongozi wa kidini kuhakikisha kuwa uvamizi wa mara kwa mara unaoshuhudiwa katika bonde la kerio pamoja na kaunti ya Laikipia unatafutiwa suluhu.