WAKAZI WATAKIWA KUHAKIKISHA WANAO WANAPATA CHANJO TRANS NZOIA.

Na Benson Aswani
Wito umeendelea kutolewa kwa umma kuwapeleka wanao kupata chanjo katika Hospitali zote za Umma Kaunti ya Trans-Nzoia kwani imebanika idadi ndogo ya wazazi wanajitokeza kuwapeleka wanao kupata chanjo hizo.
Kwenye mkao na wanahabari baada ya hamasisho kwa washikadau katika sekta ya afya muuguzi, mkuu katika Hospitali ya Saboti Millicent Mitei amesema wizara ya afya Kunti hiyo kuanzia juma lijalo litaanzisha mpango wa siku 100 kutemebelea kila boma kuhakikisha watoto wote wenye chini ya umri ya miaka 5 wanapokea chanjo hizo, wakilenga zaidi chanjo ya measeals Rubellah 2 na HPV kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka 10-14.
Aidha Mitei amesema kuwa chanjo hizo ni muhimu sana kwa watoto kwani inasaidia kuongeza kinga mwilini mbali na kuwaepusha didhi ya kuzuka kwa janga la baadhi ya maradhi hayo ambayo husababisha kupofuka au kupoza kwa watoto kutokana na makali ya maradhi hayo.