WAKAZI WAONYWA DHIDI YA KUGAWANYWA ARDHI POKOT MAGHARIBI.


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi hasa wanaoshi kwenye ardhi za jamii yani community land wameshauriwa kutoshinikiza kupewa hati miliki za ardhi hali itakayopelekea kugawanya ardhi hizo.
Akizungumza katika fisi za kamishina wa kaunti hii katibu mkuu katika wizara ya ardhi Alex Mburi amesema kuwa licha ya kuwa ni haki ya kila mmoja kugawiwa ardhi hali hii huenda ikaibua mizozo ya ardhi hasa ikizingatiwa wakazi wengi wa kaunti hii ni wafugaji.
Wakati uo huo Mburi amewataka wakazi kukumbatia mbinu ya kutumia wazee wa mitaa katika kusuluhisha mizozo ya ardhi inapoibuka badala ya kuelekea mahakamani ili kuokoa wakati pamoja na pesa ambazo huenda wakalazimika kutumia katika kesi hizo.
Kwa upande wake gavana wa kaunti hii ya pokot magharibi John Lonyangapuo amewahimiza wakazi wa kaunti hii kutokuwa wepesi wa kutumia hati miliki zao za ardhi katika kutafuta huduma mbali mbali kwani huenda hali hii ikapelekea kupoteza ardhi zao.