WAKAZI WALALAMIKIA HUDUMA DUNI KATIKA HOSPITALI YA KACHELIBA.

Na Benson Aswani
Wakazi wa eneo la Kongelai eneo bunge la Kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi wanalalamikia huduma duni katika hospitali ya Kacheliba.
Wakiongozwa na Nelly Pusha wakazi hao wamesema kuwa kwa muda sasa wamekosa huduma muhimu katika hospitali hiyo ikiwemo huduma za kupima damu pamoja na dawa, ambapo wanalazimika kutafuta huduma hizo kwingine kabla ya kushughulikiwa katika hospitali hiyo.
Wakazi hao wamedai kuwa gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo anatumia muda wake mwingi kushughulikia chama chake cha KUP huku wakazi wakihangaika kwa ukosefu wa huduma muhimu za afya wakimtaka kuchukua hatua za dharura.
Ni kauli madai ambayo yamethibitishwa na muuguzi mkuu katika hospitali hiyo Luke Kanyang’areng ambaye hata hivyo amesema kuwa ni tatizo la muda tu kwani kwa sasa zipo dawa ambazo zinasubiriwa kusambazwa katika hospitali hiyo kutoka shirika la kusambaza dawa na vifaa vya matibabu KEMSA.