WAKAZI WAHIMIZWA KUJISAJILI ILI KUPOKEA NETI.


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kujisali ili kuwa katika nafasi bora ya kupokea neti katika zoezi la kugawa neti hizo linalotarajiwa kuendelezwa na maafisa wa idara ya afya kaunti hii.
Ni wito ambao umetolewa na mkuu wa kitengo cha maji na usafi wa mazingira katika wizara ya afya kaunti hii ya Pokot magharibi Abel Koech ambaye amewataka wananchi kushirikiana na maafisa watakaoendeleza zoezi la usajili akisema watakaosajiliwa pekee ndio watakaopokea neti hizo.
Wakati uo huo Koech amewataka wakazi watakaopokea neti hizo kutozitumia katika kazi zingine kama vile kuzuia maboma yao au sehemu walikopanda mimea na badala yake kuzitumia vyema kwa shughuli inayokusudiwa ya kuzuia kuumwa na mbu ili kudhibiti kusambaa ugonjwa wa malaria.