WAKAZI WA TRANS NZOIA WATAKIWA KUKUMBATIA BIASHARA YA PORI.

Wito umetolewa kwa wenyeji Kaunti ya Trans-Nzoia wanaomiliki mashamba makubwa Kukumbatia biashara ya ufungaji wa wanyama pori kama njia moja ya kujipatia mapato, badala ya kutegemea ukuzaji wa zao la mahindi pekee.
Akihutubu kwenye hafla ya kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mbunga ya Wanyama ya Kitaifa ya Saiwa eneo bunge la Cherangani, Mshauri mkuu wa kisheria katika afisi ya naibu wa Rais Dkt Abraham Singoei amesema sheria mpya ya usimamizi wa Wanyama pori inaruhusu ufugaji wa Wanyama hao.
Kwa upande wao Msimamizi wa mbunga za Wanyama eneo la Magharibi Catherine Wambani na msimamizi wa shirika la uhifadhi wa mbuga ya Saiwa kwa jina Nyumbani Kwetu Paul Kurgata wamesema ipo haja ya wenyeji wanaopakana na mbuga hiyo ya Wanyama kubadili mbinu ya ukulima eneo ili kuzuia uharibifu wa mazingira na kuhifadhi wanyama katika mbuga hiyo.