WAKAZI WA TIATY BARINGO WAKOSA HUDUMA MUHIMU KUTOKANA NA OPARESHENI INAYOENDELEA


Wakaazi kutoka eneo la Tiaty kaunti ya Baringo wanaendelea kupitia hali ngumu ya maisha ambayo imewazonga kwa mda mrefu.
Kulingana na wakaazi hao ni kwamba wamekosa chakula na bidhaa nyingine muhimu za kimsingi.
Akizungumza na wanahabari, Mwakilishi wadi wa eneo la Silale kaunti ya Baringo Nelson Lotela amesema kuwa wakazi wa eneo hilo hawawezi kupata chakula na hata huduma zingine muhimu za afya kutokana na oparesheni ya kusaka silaha ambayo imewaathiri pakubwa wengi wao ambao hawana hatia.
Lotela aidha amesema kuwa mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu likiwemo shirika la mslaba mwekundu, lile la World Vision miongoni mwa mashirika mengine hayawezi kufika eneo hilo baada ya kuzuiliwa.
Ameongeza kuwa iwapo serikali haitatoa suluhisho basi wakaazi wengi huenda wakafariki.